Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema ushindi wa mechi zao tano za ligi kuu umewapa maandalizi mazuri kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya JS Saoura ya Algeria.
Aussems ameyasema hayo jana baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Stand United kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga.
“Ushindi huu ni muhimu kwetu kwa kipindi hiki ambacho tunajiandaa kwenda kucheza na JS Saoura.”- Alisema Patrick Aussems.
Kikosi cha Simba kimerejea jijini Dar es salaam kwa ndege kikitokea Mwanza ambako walilala baada ya kutoka Shinyanga jioni muda mfupi baada ya mchezo.
Pia Simba inatarajiwa kuondoka nchini leo jioni kuelekea nchini Algeria tayari kwa mchezo huo wa Kundi D ambao utapigwa Jumapili Machi 9, 2019.
Katika kundi hilo Simba inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 6 kwenye mechi 4 nyuma ya Al Ahly yenye alama 7 kileleni.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments