Jide Azua Gumzo Msiba wa Ruge....Afunguka na Kudai Hajali | ZamotoHabari.

Baada ya watu kuhoji sana katika mitandao ya kijamii kwanini   mwanadada Lady Jay Dee ameshindwa kufika katika msiba wa mkurugenzi wa Clouds Media baada ya msiba huo kutokea zaidi ya wiki sasa na kila mtu akiwa na masikitiko na kifo icho.

Hata hivyo baada ya kusemwa sana katika mitandao ya kijamii na watu mbalimbali, mwanadada huyo alionekana kama kuwajibu baadhi ya wanaomsema kwa kusema kuwa hajali kitu kuhusu swala hilo wala maneno yao .Na hivyo aliweka picha yake na kusema


Ikumbukwe kuwa mwanadada Lady jay dee aliwahi kusema kuwa hatokaa kukanyaga katika msiba wa Ruge au Joseph Kusaga na wao wafanye hivyo kwa sababu anaamini kuwa Ruge ndio alikuwa moja ya watu waliokuwa wakiziba sana mianya ya kazi zake kufanya vizuri nje ya nchi.

Hata baada ya kusema hayo miaka mingi iliyopita na hata kusemwa kuwa nyimbo za mwanadada huyo hazikuwa zikipigwa katika Clouds media , bifu hilo liliendelea na hata mkurugeniz huyo amekufa mwanadada huyo hakutokea msibani.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini