Kikosi cha Simba SC Chatua Salama Dubai kuwafuata Waarabu | ZamotoHabari.

Kikosi cha Simba SC Chatua Salama Dubai kuwafuata Waarabu
Wachezaji wa Simba SC, benchi la ufundi na viongozi walioambatana na timu wamefika salama Dubai ambapo inaaeleza kuwa walilala hapo usiku wa kuamikia leo kisha wataondoka kwenda Algeria.



Simba SC watacheza mchezo wa tano wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura siku ya Jumamosi Machi 9, mwaka huu.

Wekundu hao wa msimbazi watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kuwalaza JS Saoura Magoli 3-0 katika mchezo wao wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam.

Hadi sasa Simba SC wanashika nafasi ya pili kwenye kundi lao wakiwa wamejikusanyia pointi 6 kibindoni katika michezo minne waliocheza ambapo wamefungwa miwili na kushinda miwili ambapo walicheza nyumbani.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini