Katika mfululizo wa michezo katika ligi kuu nchini Uingereza, jana kumefanyika michezo mitatu na moja ya mchezo uliovuta masikio ya watu wengi ulikuwa ni mchezo uliowakutanisha Majogoo Liverpool ambao walikutana na wapinzani wao wakubwa katika mji wa Liverpool ambao pia ni majirani zao na imefikia mpaka watu kusema ni watoto wa baba mmoja Everton.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa unawalazimu Liverpool kupata ushindi kwa vyovyote vile ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kuendelea kuwa vinara wa ligi hiyo kwa kuendelea kukimbizana na Manchester City, na mwisho wa siku mchezo ukamalizika kwa sare tasa yaani sare ya kutokufungana kati ya timu hizo zenye upinzani mkubwa katika jiji hilo.
Mpaka sasa Manchester City wamekaa kileleni kwa alama 71 huku Liverpool wakiwa na alama zao 60 katika nafasi ya pili baada ya sare ya jana dhidi ya majirani zao Everton.
Na baada ya mchezo Kocha wa Liverpool Mjerumani Jurgen Klopp alionesha kutokufurahishwa na matokeo hayo ndio maana hata wakati wa Press akiwa anaongea na waandishi wa habari aliongea maneno ya hasira sana.
Klopp aliulizwa katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya mechi kama wangeweza kuongeza mshambuliaji mwingine zaidi, labda, ili kupata pointi muhimu katika mbio za kuwania cheo cha Premier League dhidi ya Manchester City.
Lakini Ujerumani huyo alisema: “Nimevunjika moyo sana juu ya swali lako. Hatuko hapa kwa ajili ya kucheza PlayStation.”
“Je! Unafikiri hatukupata nafasi za kutosha leo? Ni swali la kukatisha tamaa kwa sababu hiyo inamaanisha ni rahisi sana, nilijaribu kuwaambia Comoni boys, tujaribu mara nyingi langoni, maana tulikuja kwa ajili ya matokeo’.”
“Mshambuliaji wa ziada tu kama unakwenda porini? Unafikiri ni kama PlayStation, kuleta mshambuliaji mwingine na mabadiliko ya mpira wa miguu?” Si kama hiyo.Tuna hasira ya kutosha .. Soka haifanyi kazi kama hiyo Play Station, hatuwezi kupoteza ujasiri wetu.”
“Kumbuka City walishinda lakini walitengeneza nafasi karibia 20 lakini walipata goli moja tu, sio rahisi kama unavyofikiria”
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments