Lipumba atoa neno Lowassa kurudi CCM | ZamotoHabari.


Kitendo cha aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA Edward Lowassa kurejea CCM chamshangaza  Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

 Profesa Lipumba amesema kuwa anashangazwa na uamuzi wa Edward Lowassa kurejea CCM katika kipindi ambacho mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa gerezani.

"Lowassa amerudi CCM bila aibu. (Amerudi) wakati Mbowe bado yupo gerezani. Hakufikiria wenzake anawaachaje," alisema Profesa Lipumba.

Lipumba ambaye mwaka 2015 alijivua uenyekiti kutokana na CUF kuunga mkono Lowassa kugombea urais kwa mgongo wa vyama vinne, amesema hajashangazwa na hatua ya Lowassa kurejea CCM kwa kuwa alijua ingawa hakufahamu siku.

Mbowe pamoja na mbunge wa Tarime, Esther Matiko, yupo Segerea tangu Novemba 23, 2018 baada ya dhamana yao katika kesi ya jinai inayowakabili pamoja na viongozi wengine wa Chadema, kufutwa.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini