Lipumba Awagonganisha Mbowe,Lowassa na Maalim Seif | ZamotoHabari.



Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Profesa Ibrahim Lipumba amesema wakati wa uchaguzi Mkuu wa 2015, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alimkataa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kujiunga na UKAWA
kwa kile alichokidai kuwa alikua haaminiki.

Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho ambao ulimpigia kura yeye kukiongoza chama hicho kwa miaka mingine mitano.

Lipumba amesema, "Maalim Seif alimuita Mbowe wakutane Zanzibar baada ya kupata taarifa Lowassa hatapitishwa CCM kwa ajili ya kugombea, akamwabia unaonaje tukamkaribisha UKAWA lakini Mbowe wakati ule Mbowe alikataa kumkaribisha kwasababu alidai hawaaminiki", amesema Lipumba.

"Jambo la singi tunapoelekea kwenye uchaguzi ujao tunahitaji ushirikiano wa dhati sio ushirikiano wa kinafki wa kukidhoofisha vyama vingine" ameongeza Lipumba

Kwa sasa chama hicho kimekuwa na mpasuko wa kiuongozi baada ya kuwepo kwa pande mbili za uongozi ikiwemp upande unaomuunga mkono Profesa Ibrahim Lipumba na Upande unaomuunga mkono Maalim Seif Sharif Hamad
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini