Mabadiliko ya kanuni za mpira kwa msimu ujao 2019/2020 . | ZamotoHabari

The International Football Association Board (The IFAB) , imebadilisha baadhi ya kanuni za mchezo wa soka kwenye kikao kilichofanyika wiki iliyopita nchini Scotland . Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:-

1. KUTAKUWA HAKUNA MREJESHO KUTOKANA NA PIGO LA PENATI

Mchezo utasimama kwa kuanzishwa kama penati imeokolewa au imegonga mwamba , hii ina maana hakuna tena nafasi ya kufuata mpira na kufunga ( Rebound ) kwa maana hiyo wachezaji hawatokuwa na uhitaji wa kujipanga nje ya 18.

2.MPIRA KUCHEZWA NA MKONO.

Kuanzia Juni mosi goli litakalofungwa ambalo limegusa mkono wa mchezaji kwa maksudi au bahati mbaya ( Mfungaji ) halitakubaliwa.

3.MABADILIKO YA MCHEZAJI 

Mchezaji ambaye atakuwa anafanyiwa mabadiliko ataruhusiwa kutoka kupitia upande wowote ule wa uwanja 

4. GOAL KICK 

Mchezaji ataruhusiwa kugusa mpira hata ndani ya eneo la 18 kutoka kwa kipa , ambapo sasa hivi ni mpaka mpira utoke kwenye 18 ndio unaruhusiwa kuugusa.

5. KADI KWA MAKOCHA.

Makocha sasa nao watakuwa wanaoneshwa kadi ya njano na nyekundu tofauti na sasa hivi wanaambiwa tu toka kwenye eneo la benchi la ufundi.

6.  KWENYE UKUTA WA KUZUIA MIPIRA ILIYOKUFA

Wachezaji wa upande ambao wanapiga mipira iliyokufa ( freekick ) hawatoruhusiwa kwenda kujumuika kwenye ukuta wa timu ambayo inazuia mipira hiyo , tofauti na sasa huwa wanachanganyika kama kuwatoa mchezoni.

7. PENATI .

Magolikipa wataruhusiwa kuweka mguu mmoja tu kwenye mstari na huo mwingine wataamua wao wenyewe waweke wapi , tofauti na sasa kwamba miguu yote lazima iwe kwenye mstari wakati anapigiwa penati.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini