Mabaraza ya Mitihani ya Afrika mashariki yaungana | ZamotoHabari.

Mabaraza na Bodi za mitihani za nchi za Afrika mashariki kwa pamoja zimekubaliana kuanzishwa kwa umoja wa nchi za Afrika Mashariki katika tathmini ya elimu.

Kufuatia uamuzi huo Katibu Mkuu wa baraza la taifa la mitihani nchini Tanzania, Dkt.  Charles Msonde ameteuliwa kuwa Rais wa Umoja huo.

Akizungumza na wanahabari wakati akitambulisha umoja huo, Dkt. Msonde amesema kuwa, umoja huo utasaidia kuongeza ufanisi kiutendaji katika nchi za Afrika mashariki.

"Kwa pamoja leo tutasaini Katiba yetu itakayoongoza umoja huu ambao mimi ndio Rais baada ya wao kunipendekeza na katibu wangu anatokea nchini Uganda huku mhasibu akiwa ni Mkenya", amesema Dkt. Msonde.

Kwa upande wake Katibu wa umoja huo kutoka nchini Uganda,  Dan Odongo amesema kuwa umoja huo utakuza na kuimarisha nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuzuia udanganyifu katika kipindi cha mitihani ya kitaifa.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini