MAPYA YAIBUKA MCHUNGAJI ALIYEDAI KUFUFUA MTU


Kipindi cha habari za uchunguzi kinachorushwa na kituo cha Shirika la Utangazaji Afrika Kusini (SABC) kinachoitwa Cutting Edge, kimebaini mapya kuhusu mchungaji Alph Lukau.

Kipindi hicho ambacho kimerushwa siku ya Jumanne ya wiki hii, kimebaini kuwa mchungaji huyo mwenye asili ya Kongo amekuwa akiwafuata watu msikini na kuwalipa, ili waende kutoa ushuhuda wa uongo kwenye kanisa lake, kwa ajili ya kuvutia watu wengi zaidi.

Uchunguzi wa kina wafanyika 

Uchunguzi umebaini kuwa watu wengi waliongea tofauti na kile walichotarajia, kwa kuumbua matendo mabaya ya mchungaji huyo aliyedai kumfufua mtu hivi karibuni.

Samantha Revesai ambaye aliaminiwa kuwahi kuponywa UKIMWI na mchungaji huyo, amefunguka na kusema kwamba mchungaji Lukau alimfuata na kupanga naye dili, na kisha kwenda kanisani kujifanya ni muathirika wa UKIMWI ili amuombewe.

"Sikuwa muathirika na wala sijawahi kuwa muathirika, walitaka niigize kama mtu aliyeathirika na UKIMWI, kisha mchungaji akaniombea na kuniponya, ili wavutie watu wengi waje kanisani”,amesema Samantha.

Lakini licha ya habari hizo zote mwanasheria wa kanisa hilo bado hajazungumza lolote, na msemaji wa kanisa hilo Bui Gaca amekanusha taarifa hizo na kusema kwamba ni uongo unapangwa kumchafua Mchungaji Lukau.

Mchungaji Lukau alipata umaarufu zaidi mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya kutrend kwa habari ya kumfufua mtu, ambaye baadaye ilikuja kujulikana na mwenyewe kukiri kuwa mtu huyo hakuwa amefariki dunia.


Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini