MASHINDANO YA BAMMATA SOKA JKT WAAGA KWA KISHINDO | ZamotoHabari


Nahodha wa Kanda ya Magereza Sajini Tausi Abdul akipambana na Private Ester Lisu wa Ngome wakati wa Mchezo wao katika Michauano ya BAMMATA kuwania nafasi ya pili katika Mchezo huo Ngome ilishinda Magereza vikapu 68 kwa 60 . Picha na Luteni Selemani Semunyu.

Mchezaji wa Kanda ya Magereza Sajini Mary Kimiti akipambana na Private Ester Lisu wa Ngome wakati wa Mchezo wao katika Michauano ya BAMMATA kuwania nafasi ya pili katika Mchezo huo Ngome ilishinda Magereza vikapu 68 kwa 60 . Picha na Luteni Selemani Semunyu.


Wachezaji wa Mpira wa Wavu kutoka Magereza na JKT wakichuana wakatika wa Michuano ya Majeshi BAMMATA katika Mchezo huo Magereza walishinda Seti tatu kwa moja Picha na Luteni Selemani Sem unyu.



Na Luteni Selemani Semunyu

Mashindano ya Majeshi Tanzania BAMMATA yameendelea kushika kasi huku timu ya Soka ya JKT ikiaga mashindano hayo kwa mwaka 2019 kwa kishindo baada ya kuifunga Zimamoto magoli 10 kwa Moja.

Matokeo hayo yamejitokeza katika mchezo wa kufunga Dimba uliochezwa katika Dimba la Uhuru licha ya Timu hizo zote hazikuwa na nafasi ya kuingia katika Hatua ya Nusu Fainali.

Katika Soka sasa Mchezo kati ya Ngome na Magereza unaotarajiwa kuchezwa kesho katika Dimba la Uhuru utaamua nani wa kucheza na Polisi na nani kucheza na SMZ katika hatua ya Nusu Fainali.

Katika Ridha atika mchezo mwingine Mpira wa Kikapu Wanawake mchezo uliokuwa ukiamua mcshindi wa Pili Ngome wameibuka na Ushindi kwa Vikapu 68 kwa 60. Katika Mpira wa Wavu wanawake Magereza wameifunga JKT kwa seti tatu kwa Moja huku kwa Upande wa Wanaume Ngome wameifunga Polisi Seti tatu bila.

Katika Shabaha pistor wanawake mshindi wa Kwanza Pc Pili Mkama wa pili PC Salvina Mhiche na PC Bertha Jonathan wote wa Polisi.

Kwa Upande wa Wanaume Sajini Kenya Kiula wa Polisi wa pili ni Sajini Jumanne Wambura wa Ngome na watatu ni PC Joseph Mwenda Polisi.

Kwa Upande wa Rifle Wanawake ni Private Elizabeth Kibondo Ngome wa pili ni Mteule Daraja la Pili Sophia Ramadhani wa Ngome na PC Sharifa Kibwana Ally wa Polisi huku kwenye Riadha relay wanaume Mita 400 Timu ya Ngome imeibuka na Ushindi.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini