MASHINDANO YA BAMMATA SOKA JKT WAAGA KWA KISHINDO | ZamotoHabari

Na Luteni Selemani Semunyu
MASHINDANO ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) yameendelea kushika kasi huku timu ya Soka ya JKT ikimaliza mashindano hayo kwa mwaka 2019 kwa kishindo baada ya kuifunga Zimamoto magoli 10 kwa Moja.

Matokeo hayo yamejitokeza katika mchezo wa kufunga Dimba uliochezwa katika Dimba la Uhuru, licha ya Timu hizo zote hazikuwa na nafasi ya kuingia katika Hatua ya nusu Fainali. Katika Soka  Mchezo kati ya Ngome na Magereza unaotarajiwa kuchezwa kesho katika Dimba la Uhuru utaamua nani wa kucheza na Polisi na nani kucheza na SMZ katika hatua ya Nusu fainali.

Aidha katika riadha na  Mpira wa Kikapu  kwa wanawake mchezo katika mchezo huo Ngome waliibuka mshindi wa pili kwa Vikapu 68. Katika Mpira wa Wavu   wanawake Magereza wameifunga JKT kwa seti tatu kwa moja huku kwa upande wa Wanaume  Ngome wameifunga  Polisi Seti tatu bila.

Katika Shabaha pistor wanawake mshindi wa Kwanza Pc Pili Mkama wa pili PC Salvina Mhiche na PC Bertha Jonathan wote kutoka kikosi cha Polisi. Kwa Upande wa Wanaume Sajini Kenya Kiula wa Polisi aliibuka nafasi ya kwanza huku nafasi ya  pili ikishikwa Sajini Jumanne Wambura wa Ngome na watatu ni PC Joseph Mwenda Polisi.


Kwa Upande wa Rifle  Wanawake nafasi ya kwanza ilichukuliwa na  Private Elizabeth Kibondo kutoka Ngome wa pili ni  Mteule Daraja la Pili Sophia Ramadhani wa Ngome na PC Sharifa Kibwana Ally wa Polisi huku kwenye Riadha relay wanaume Mita 400 Timu ya Ngome imeibuka na Ushindi.
Nahodha wa Kanda ya Magereza Sajini Tausi Abdul akipambana na Private Ester Lisu wa Ngome wakati wa Mchezo wao katika Michauano ya BAMMATA kuwania nafasi ya pili katika Mchezo huo Ngome ilishinda Magereza vikapu 68 kwa 60 . Picha na Luteni Selemani Semunyu.
Mchezaji wa Kanda ya Magereza Sajini Mary Kimiti akipambana na Private Ester Lisu wa Ngome wakati wa Mchezo wao katika Michauano ya BAMMATA kuwania nafasi ya pili katika Mchezo huo Ngome ilishinda Magereza vikapu 68 kwa 60 . Picha na Luteni Selemani Semunyu.
Wachezaji wa Mpira wa Wavu kutoka Magereza na JKT wakichuana wakatika wa Michuano ya Majeshi BAMMATA katika Mchezo huo Magereza walishinda Seti tatu kwa moja Picha na Luteni Selemani Sem unyu.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini