Matumizi ya dawa za kutuliza maumivu kiholela yatajwa kuchangia magonjwa ya Figo | ZamotoHabari.


Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa miongoni mwa vitu vinavyochangia uharibifu wa Figo ni matumizi ya dawa za kutuliza maumivu mara kwa mara.

Dkt. Ndugulile amesema hayo wakati akizungumzia maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani Jijini Dodoma iliyobeba kauli mbiu isemayo Afya ya Figo kwa kila mmoja kwa kila mahali.

Amesema kuwa watanzania wengi wamekua wakitumia Dawa kiholela bila ya kupima na kufuata ushauri wa Daktari hasa matumizi ya Dawa za maumivu kila wanapohisi kupata maumivu ya kichwa kwani hivi sasa wagojwa wa Figo wanaendelea kuongezeka nchini.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini