MREMBO Pretty Kind Akiri Kuwa na Tabia ya Umbea "Nimesutwa Sana Sababu ya Umbea Wangu" | ZamotoHabari.

MSANII wa filamu za Kibongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amefichua siri yake kwamba alipokuwa mdogo alikuwa mbeya kiasi cha kuwafanya watu kumuogopa pale walipokuwa wakiongea mambo yao.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Prett Kind alisema kuwa alikuwa akipenda kudakia mambo ya watu wakiwa wanaon­gea na kuyaanika, kitu ambacho kiliwakera sana.

“Yaani umenikumbu­sha mbali kweli, baba yangu alikuwa hanipendi kwa sababu ya mashosti, nilikuwa na marafiki wengi nawajaza nyum­bani lakini ndugu zangu walikuwa hawanipendi kwa umbeya, yaani nimesutwa sana kwa tabia hii ya umbeya,” alisema Pretty Kind.

Stor: Hamida Hassan


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini