Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
BAADA ya Mamlaka ya hali ya hewa nchini kutoa tahadhari juu ya mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka wananchi kuanza kuchukuwa tahadhari mapema katika kukabiliana na majanga ya mafuriko huku akiwataka wakazi wa mabondeni na walioko pembezoni mwa mito kuhama katika maeneo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Makonda amesema kuwa ujenzi holela na tabia ya watu kutupa taka kwenye mifereji inayopitisha maji ya mvua na mito ndio chanzo kikubwa cha mafuriko hivyo amewahimiza wananchi kuacha mara moja tabia hiyo huku akiwataka wananchi kumripoti kwa wenyeviti wa mtaa kwa yeyote atakayekaidi hilo.
Aidha Makonda ametoa siku saba kwa wakala wa barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kuhakikisha wanaziba viraka katika barabara kwakuwa vimekuwa usumbufu na kero kwa watumiaji wa barabara huku akiwaagiza TANROAD kusafisha miundombinu ya Mito,mitaro na madaraja yaliyoziba kwa usalama zaidi.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments