Sexy lady wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ (26), ameshtua wengi, Ijumaa limedokezwa.
Mshtuko huo unakuja siku kadhaa baada ya Nandy kumpoteza bosi na mtu wake wa karibu, Ruge Mutahaba (49) aliyefariki dunia Februari 26, mwaka huu.
AMEHAMA
Mapema wiki hii, Gazeti la Ijumaa lilifunga safari hadi nyumbani kwa mwanamuziki huyo, Masaki jijini Dar kwa ajili ya kufanya naye mahojiano ndipo likakutana na habari hizo za kushtua kuwa amehama kwenye mjengo wake wa kifahari ambao miezi kadhaa iliyopita aliunadi pamoja na magari yake makali. Baada ya Gazeti la Ijumaa kufika nyumbani hapo lilipewa taarifa na majirani kuwa; “Nandy amehama jamani”.
IJUMAA KAZINI
Hata hivyo, Gazeti la Ijumaa huwa ni sikivu, lakini hutaka kuthibitisha mambo yake hivyo lilizama kazini kujua kama kweli Nandy amehama au la.
Ndipo lilipoamua kugonga geti ili kujiridhisha ambapo baada ya kugonga kwa muda mrefu huku kelele za mbwa mkali zikisikika, alitoka mwanadada mwenye asili ya Kiarabu na kusema; Nasikia mnamuulizia Nandy, hapa amehama.”
“Kwa sasa ninaishi mimi na familia yangu hapa, huyo mtu mnayemsema alishahama ndiyo tukaingia sisi,” alisema dada huyo shombeshombe.
MLINZI WA NANDY
Hata hivyo, wakati Gazeti la Ijumaa likiendelea kujibizana na dada huyo alitoka mlinzi kwenye geti lingine ambaye ndiye alikuwa akimlindia Nandy alipokuwa akiishi hapo.
Baada ya kumuona mlinzi huyo na kwa kuwa Ijumaa linamfahamu ndipo likaachana na yule dada wa Kiarabu kisha ‘kudili’ na mlinzi huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Rashid.
Mlinzi: Karibuni, nimewasikia mnagonga geti hapa muda mrefu, mnamuulizia Nandy!
Ijumaa: Ahsante. Ni kweli tunamuulizia Nandy ila hatujampata, tumeambiwa amehama, unaweza kujua amehamia wapi?
Mlinzi: Ni kweli Nandy amehama hapa. Amehamia (akataja sehemu aliyohamia). Baada ya kuhama ndipo amekuja Mwarabu ndiye amepanga nyumba hii.
Ijumaa: Sasa kwa nini amehama? Kwa sababu nyumba hii ni nzuri sana!
Mlinzi: Mimi siwezi kujua, lakini nahisi amekwenda kutafuta unafuu wa kodi ya nyumba.
Ijumaa: Kwani hapa alikuwa analipa shilingi ngapi?
Mlinzi: Alikuwa analipa dola 750 za Kimarekani (zaidi ya shilingi milioni 1.7 za Kitanzania.)
NANDY ANASEMAJE?
Gazeti la Ijumaa lilimtafuta Nandy mara kadhaa kupitia simu yake ya kiganjani bila kupokelewa. Alipopatikana mara ya mwisho aliomba aachwe kwanza kwani kwa sasa hayupo tayari kuzungumza chochote hivyo jitihada za kumapata zinaendelea.
TUJIKUMBUSHE
Nandy aliripotiwa kuhamia kwenye nyumba hiyo mapema mwaka jana huku kukiwa na madai ya kupangiwa na mwanaume, jambo ambalo alilikanusha vikali. Mwishoni mwa mwaka jana, Nandy aliwakabidhi wazazi wake mjengo mpya aliowajengea jijini Dar huku akionesha magari yake likiwemo aina ya Benz.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments