Ommy Dimpoz Awaomba Msamaha Aliowakosea Kwakuwa Anataka Kuwa na Amani kati Yao | ZamotoHabari.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ommy Dimpoz amewataka watu wote ambao amewakosea kumsamehe, kwani anataka kuwa na amani kati yao.


Ommy Dimpoz amesema hayo alipokuwa akitambulisha video ya wimbo wake mpya wa 'You are the best' kwenye FNL ya East Africa Television, na kusema kwamba hata kama kuna mtu anahisi amemkosea na hajui, anamuomba radhi ili waweze kuyafurahia maisha, kwani maisha ni mafupi sana.

Alichokiongea Ommy Dimpoz kuhusu msahama


“Mimi kila siku niko peace na kila mtu, lakini huwezi ukalazimisha uongee na mtu fulani, mimi sina tatizo, kwa yeyote anayehisi Ommy nina tatizo naye, mimi sina tatizo, maisha yenyewe ni mafupi haya, na kama kuna ambaye nimemkosea, naomba samahani anisamehe, mimi binadamu sijakamilika, nisamehe, huwezi kuomba msamaha mmoja mmoja kwa sababu inawezekana kuna mtu hujui kama umemkosea akaiweka moyoni, tusameheane”, amesema Ommy Dimpoz.

Hivi karibuni msanii huyo alipitia kipindi kigumu cha maradhi, na kitu ambacho amekiri kuwa kimempa fundisho kubwa juu ya maisha ya binadamu kuwa si kitu hapa duniani.





Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini