Picha : SAFARI YA MWISHO YA MWANDISHI WA DW CHARLES OLE NGEREZA JIJINI ARUSHA

 Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoani Arusha Cloud Gwandu akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha- APC) Charles Ole Ngereza.
 Mweka hazina wa Klabu ya  waandishi wa habari Mkoani Arusha Pamela Mollel akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya mwenyekiti wa (APC)
 Mratibu wa APC Arusha Seif Mangwangwi akilia kwa huzuni mara baada ya mwili wa Charles Ngereza ulipowasili waliopo pembeni yake ni baadhi ya waandishi wa habari wakiwa msibani. 
 Baadhi ya Viongozi wa kanisa la Sent-James Anglican PASTOR, MICHAEL GILAISI  QAWOGA  UIJILISTI NA UMISSION wakiongoza ibada nyumbani ya maziko ya aliyekuwa mwandishi wa Habari wa Idhaa ya Kiswahili DW  Charles Ole Ngereza.
Watoto wa marehemu Charles Ngereza, Faith na Fransis wakiwa kanisani.
 Mary Mwita Mke wa marehemu Charles Ngereza akiwa kanisani ibada ikiwa inaendelea.
 Mke wa Marehemu Charles Ngereza Mary Mwita akiwa ibadani katika kanisa la Anglikana Sent. James Arusha
Mjane Mary Mwita akielekea Jeneza kuuaga mwili wa mume wake kwa mara ya mwisho
 Waandishi wa habari wakiwa msibani katika viwanja vya shule ya sekondari Baraa Jijini Arusha.
Baadhi ya waandishi wa habari Jijini Arusha wakielea katika viwanja vya Shule ya Sekondari Baraa katika kata ya baraa ambapo shughuli ya  za Ibada na taratibu zingine zinafanyika. 




Na Vero Ignatus, Arusha
'Kwaheri Charles Ngereza  Kiongozi wetu' Haya ni maneno ya Wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Arusha wakati wa kuuaga mwili wa mpendwa wao  kwa mara ya mwisho.

Marehemu Charles Ngereza hadi anafariki  alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa  Arusha ambapo aliwahi kufanya kazi katika vyombo mbalimbali ikiwemo Radio Five ya Jijini Arusha,Itv &Radio one hadi mauti inamkuta alikuwa mwakilishi wa Idhaa ya Kiswahili ya DW Ujerumani.

Ameshikilia nafasi hiyo tangu mwaka 2005 hadi umauti ulipomkuta, Katika uhai wake Charles Ngereza amekuwa  akifanya kazi kwa uadilifu na siku zote amekuwa mtu wa kushauri zaidi badala ya kuhoji, alisema Claude Gwandu mwenyekiti wa APC.

Akiwa mmoja wa wanaounda kamati ya utendaji  ya Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha Ngereza amekuwa kiunganishi kikubwa kati ya waandishi wa habari wa ndani na nje na kwa hapa tutamkumbuka zaidi katika kutoa ushauri na kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
Siku zote Ngereza amekuwa akiamini katika diplomasia, hata pale mambo yanapokwama amekuwa msaada mkubwa kuhakikisha suluhisho inapatikana na katika kamati zetu pale ndani ya APC amekuwa akishirikishwa kwenye kamati  mbalimbali ikiwemo ile kamati ya  nidhamu na maadili pale mambo yanapoonekana hayaendi sawa.

"Sisi kama wanahabari wa Mkoa wa Arusha tunasema tumempoteza mtu muhimu sana katika tasnia ya habari na kwa msemo wa sasa hivi tunaweza kusema tumepoteza ‘jembe’ na hakika pengo lake halitazibika japo mambo ya Mungu ni mengi tutaendelea kumuomba yeye ili aweze kupatikana mfano wa Ngereza",alisema mweka hazina wa APC Pamela Mollel. 

"Ngereza alikuwa ni zaidi ya rafiki kwa kuwa alikuwa akishiriki hata kwa mambo ya kijamii ndani ya APC tumekuwa na miradi ya kijamii ikiwemo kupanda miti katika shule za kata, Ngereza amekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi hizi ili kuona jamii na yenyewe inafaidika na uwepo wa Chama wa waandishi wa habari mkoa wa Arusha.

Wapendwa kwa ufupi nipende tu kusema yapo mambo mengi sana ambayo Ndugu yetu, kaka yetu Charles Ngereza ameyafanya lakini wacha tuishie hapa kwa ufupi sababu hata kama tukisema tuendelee kuyasema hapa hatutaweza kuyamaliza,kikubwa sisi kama wanahabari Mkoa wa Arusha, wafanyakazi wenzake tunaahidi tutaendelea kuyaenzi yale yote aliyoyaacha ili kuendeleza umoja na ushirikiano aliokuwa akiusisitiza.

Tunaamini Charles amefariki mwili lakini roho yake bado ipo mioyoni mwetu, kwa kuwa hata wakati anaugua anapambania afya yake kila siku tulimsihi na kumpatia faraja na hakika aliamini katika Mungu.

Tuliamini alipokwenda India kupata matibabu atarejea akiwa mzima na  kuendelea katika mapambano yetu ya kila siku lakini alirejea akiwa ameendelea kudhoofu",alisema Mustafa Leu Katibu wa Apc

Akiongoza ibada ya mazishi mchungaji wa kanisa la Anglikana ametoa angalizo kwa ndugu jamaa na marafiki kuwa makini katika kipindi hicho cha majonzi na kuwataka wasijesababisha msiba mwingine baada ya huo kwa maneno yasiyo ya hekima watakayoyatoa kwa mjane na watoto walioachwa.

"Mara nyingi msiba unapotokea ndipo watu wengi hijitokeza haswa ndugu na kuanza kuzungumza hovyo bila hekima kaa kimya ,wacheni kuzungumza hovyo, wapendwa msimpe shetani nafasi kwenye misiba ya watu"

Akitoa salamu za rambirambi mkuu wa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Lengai Ole Sabaya amesema kuwa marehemu alikuwa mpatanishi alikuwa hapendi kuona ugomvi unatokea. 

Kama wanahabari ndugu jamaa na marafiki zake niwape pole  tamaa tuliamini kila jambo linaletwa kwa mapenzi ya Mungu, tulikaa na kushauriana namna nyingine ambapo mwenzetu ataweza kupata tiba lakini wakati tukiwa kwenye mikakati hiyo Charles alizidiwa na kukimbizwa hospitali na baadae alifariki dunia.

 Inatia uchungu sana lakini hamna namna, tunasema yote ni Mapenzi ya Mungu. Nenda Charles tuko nyuma yako.

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini