Jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma limekamata magari matatu yanayoaminika ya wizi likiwamo lori la mizigo ambalo limekuwa likitumika katika matukio ya uhalifu katika mikoa mbalimbali nchini pamoja na bastola moja.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto, tukio la kwanza wamekamata gari mbili aina ya Toyota Prado zilizokuwa zikiuzwa kwenye moja ya nyumba za kulala wageni, moja wapo likiwa na namba za usajili T777 CVL huku jingine likiwa halina namba.
Aidha Kamanda Muroto amesema katika tukio jingine jeshi hilo limefanikiwa kukamata bastola moja iliyokuwa imefukiwa ardhini eneo la barabara ya kuelekea Iringa.
Baadhi ya watu ambao walijitokeza ili kutambua lori ambalo lilitajwa kuhusika kwenye matukio mbalimbali ya kihalifu ambapo nao miongoni mwa waathirika wa matukio ya kuibiwa.
0 Comments