Polisi wamuachia Dudu Baya kwa dhamana | ZamotoHabari.


Jeshi la Polisi limemuachia kwa dhamana msanii wa Bongo Fleva, Godifrey Tumaini a.k.a Dudu Baya baada ya kumshikilia kwa kile kilichoelezwa ni matumizi mabaya ya mitandao.

Kamanda wa polisi Kinondoni, Mussa Taibu amesema licha ya kumuachia kwa dhamani bado upelelezi unaendelea ingawa hakuweka wazi ni lini msanii huyo ataripoti tena Polisi.

Dudu Baya ameshikiliwa kwa saa kadhaa katika kituo cha Polisi Oysterbay Dar es Salaam.

Hatua hiyo ilifikiwa mara baada ya Dudu Baya kutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kutoa lugha isiyofaa kimaadili kwa Marehemu Ruge.

Mapema jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe aliliagiza Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kushirikiana na Polisi kuhakikisha wanamkamata msanii huyo kwa kosa la kukashifu na kutoa lugha za kejeli kwa Marehemu Ruge Mutahaba.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini