Queen Darleen: Baba alikuwa na pesa hata ukampa vipi hatosheki, Diamond anawasiliana naye sana | ZamotoHabari.

Dada yake Diamond Platnumz, Queen Darleen amekanusha taarifa ambazo zilizagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba wamemtelekeza baba yao akiwa mgonjwa.


Wiki iliyopita katika mitandao ya kijamii zilikuwa zinasambaa video zikimuonyesha mzee huyo akilalamika huku akidai kwa sasa ni mgonjwa na anahitaji msaada.

Akiongea na Wasafi TV, Darleen amedai picha mbaya za mzee huyo ambazo zinasambaa mitandaoni ni zamani sana.

“Mzee tunampigia simu na kuzungumza naye mara kwa mara lakini sasa yeye anachokitaka uende na ukifika atakutembeza kwa marafiki zake wote sasa ni kitu ambacho hakiwezekani. Na zile picha anaonekana anaumwa nizatoka mwaka 2015, mwenyewe nilivyoziona nilishituka na nilichukia sana,” alisema Darleen.

Aliongeza, “Baba ni mtu ambaye alikuwa na hela, lakini hela yake mwenyewe kaitumia na imekwisha hata nikampatia ya kwangu haitaweza mtosha. Kwa hiyo pale tunapojaaliwa kumpa tunampatia, hatuwezi ‘kufosi’jamii kiambia baba yetu sisi tunamfanyaia hichi na hichi,”
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini