Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amezisamehe kodi gari mbili za kubebea wagonjwa (Ambulance ) aina ya Mercedes Benz kwa ajili ya Hospital za Halmashauri mbili za Ortumet iliyopo Arusha Dc na Tengeru iliyopo halmashauri ya Meru.
Mhe. Magufuli amefikia hatua hiyo kufuatia ombi la Mkuu wa wilaya ya Arumeru kwa Katibu wa NEC itikadi na uenezi Ndugu Humphrey Polepole ambae pia ndie mlezi wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Arusha alipofanya ziara katika wilaya ya Arumeru kujionea kazi mbalimbali za utekelezaji wa ilani ya chama katika wilaya ya Arumeru ambapo Dc Muro alimuomba Ndugu polepole awaombe kwa Mhe Rais Magufuli ambae pia ni Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Taifa ili waweze kupata msamaha wa kodi.
Akizungumza mara baada ya Mhe. Rais Magufuli kukubali kuzisamehe kodi ambulance hizo za kisasa ambazo zimepatikana kwa jitihada za Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Ndugu Jerry Muro akishirikiana na mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Dkt Wilson Charles Mahera kutoka kwa marafiki wa asasi inayoshirikiana na wajerumani.
Ndugu polepole amesema Mhe Rais katika kuhakikisha anaendelea kuboresha sekta ya afya katika wilaya ya Arumeru pamoja na kutoa zaidi ya bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vya Usa river Halmashauri ya Meru na Nduruma pamoja na mbuyuni Halmashauri ya Arusha pia ameelekeza magari hayo ya wagonjwa yapelekwe kwenye hospital hizo mbili za wilaya ambapo yamesamehewa kodi na kuingizwa katika mfumo wa vifaa vya hospital hizo.
Dc Muro amemshukuru sana Mhe Rais Magufuli kwa kukubali kuwasaidia kusamehe kodi magari hayo , ambapo Kupatikana kwa magari haya mawili ya kubebea wagonjwa kumeendelea kuonyesha dhamira ya dhati ya Mkuu kuu wa wilaya ya Arumeru ya kuwahudumia wananchi wa Arumeru baada ya kukabidhi gari lingine la doria kwa jeshi la polisi wilaya ya Arumeru ambalo kimekarabatiwa kwa juhudi za mkuu wa Wilaya na wadau wa maendeleo.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments