SELOU MARATHON KUFANYIKA KWA MARA YA KWANZA MKOANI MOROGORO AGOSTI 25 MWAKA HUU | ZamotoHabari

Na Agness Francis, blogu ya jamii.

UZINDUZI wa maandalizi ya mbio za riadha Selou marathon umefanyika leo ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kufanyika mkoani Morogoro agosti 25 mwaka huu, lengo likiwa ni kukuza utalii wetu wa ndani na nje ya nchi pamoja na kujenga afya.

Mgeni rasmi ambaye ni muaakilishi wa mkurugenzi wa baraza la michezo Taifa Neema Msitu, akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi huo leo Jijini Dar es Salaam ambapo ametoa wito kwa watanzania kujitokeza kushiriki mbio hizo za Selou marathon itakayofanyika mkoani Morogoro pamoja na kushiriki michezo yote kwa ujumla.

"Michezo inajenga mwili na afya na kutupa uhai hivyo basi watanzania tuweke utamaduni wa kufanya mazoezi,pia tukijumuika kwa pamoja kushiriki mbio hizo tutakuza utalii wetu na uchumi pia"amesema Neema Msitu.

Aidha mratibu wa Mratibu wa Selou Marathon Rehema Jonas amesema kuwa uzinduzi wa mbio hizo inahazina kubwa ya watu wanaopenda michezo na kwa kutambua hilo wameamua kuchukua jukumu la kuandaa mbio za riadha mwaka huu mkoani morogoro.

"Morogoro ni Mkoa unaofikika kiurahisi zaidi nataraji watu wengi kutoka sehemu mbali mbali watajitokeza kuja kujumuika nasi mbio ambazo zitaanzia kilimota 21,kilomita 10,kilomita 5 ambazo ni za furaha pamoja na mbiao za kilomita 2 na nusu kwa ajili ya watoto." amesema Mratibu huyo.

Hata hivyo mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Selou marathon Emmanuel Kajula pia ameongezea kuwa lengo la kuandaa mbio hizo ni kutaka kuchochea na kukuza maendeleo ya mbio za riadha nchini Tanzania, ambapo ameeleza kuwa maendeleo ya mchezo huo hautafika mbali kama hakutakuwepo na waandaaji wa uhakika.

Nao mabalozi wa Selou marathon Msanii wa kizazi kipya Barnaba boy pamoja na mchekeshaji Tabu mtindiga wametoa wito kwa wasanii na vijana wenzao kuunga mkono mandalizi ya mbio hizo mpaka zitakapofikia kilele chake agosti 25 mwaka huu.
Mgeni rasmi  ambaye ni  muaakilishi wa mkurugenzi wa baraza la michezo Taifa Neema Msitu,akikata utepe akiashiria maandalizi ya uzinduzi wa Selou Marathon yamezinduliwa rasmi leo Jijini Dar es Salaam
 Mgeni rasmi  ambaye ni  muakilishi wa mkurugenzi wa baraza la michezo Taifa Neema Msitu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Selou Marathon leo Jijini Dar es Salaam ambapo mbizo hizo zitafanyika Mkoani Morogoro agosti 25  mwaka huu.
 msanii wa kizazi kipya Barnaba boy, ambaye pia mi balozi wa mbio za Selou marathon  akizungumza na vyombo vya habari  wakati wa uzinduzi huo leo Jijini  Dar es Salaam.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini