Stand United yafunguka kuimaliza Simba SC | ZamotoHabari.


Uongozi wa benchi la ufundi la Stand United, umeweka wazi mipango yake iliyojiwekea kwa ajili ya kuhakikisha timu hiyo inaibuka na ushindi katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ush­indani mkubwa ambapo mbinu hizo zinahusiana na timu ya Yanga ambayo ni mahasimu wakubwa wa Simba.

Kikosi cha Stand United Jumapili hii kinashuka uwanjani kupambana na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bilali ameliambia amesema kuwa wamejipan­ga vilivyo kwa ajili ya mechi hiyo na mbinu watakazotu­mia kupata ushindi katika mechi hiyo hazitakuwa na tofauti sana na zile wali­zozitumia dhidi ya Yanga na wakafanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0.

“Tunaiheshimu sana Simba, lakini katika mechi yetu ya Jumapili tutahakiki­sha tunaibuka na ushindi kutokana na mikakati yetu tuliyojiwekea.

Simba kwa sasa ipo nafasi ya tatu katika msi­mamo wa ligi kuu ikiwa na pointi, 48 wakati Stand United yenyewe ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 33. Yanga ndiyo inayoongoza msimamo huo ikiwa na pointi 61.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini