TAWA YAADHIMISHA SIKU YA WANYAMAPORI DUNIANI KWA KUTOA ELIMU KWA WATANZANIA KUHUSU WANYAMAPORI


Kamishna Mhifadhi wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) Dkt. James wakibara (wa katikati) akizungumzia mambo mbalimbali kuhusiana na siku ya wanyamapori duniani na kutoa elimu kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu wanyama, ofisi ndogo ya Wizara na maliasili na utalii Dar es Salaam.
Naibu Kamishna - Utalii na Huduma za Biashara Bw. Imani R. Nkuwi(kulia) akiwa anaelezea taratimbu mbalimbali za kufuata kupata vitalu vya uwindaji na kusisitiza kuwa hivi karibuni vitalu vyote vitapigwa mnada kwa njia ya mtandao ambapo itasaidia mtu yeyote popote duniani kuweza kupata bila kufika sehemu husika, kushoto ni Kamishna Mhifadhi wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) Dkt. James wakibara
Kamishna msaidizi mwandamizi anayeshughulukia biashara na huduma Bw. Zahoro A. Kimwaga akielezea fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana katika mapori ya hifadhi. 
Mkutano na waandishi wa Habari ukiwa unaendelea 
 ***
Kila mwaka ifikapo Tarehe tatu mwezi wa tatu dunia nzima huazimisha siku ya wanyamapori, siku hiyo imewekwa mahususi ili kuhakikisha wanayamapori wanakaa katika mazingira mazuri na salama.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kuadhimisha siku hiyo Kamishna Mhifadhi wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) Dkt. James Wakibara alisema kuwa TAWA ni shirika la Umma na mtoto aliyekuwa idara ya wanyamapori Tanzania ambayo ipo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo, idara ya wanyamapori itaendelea kushughulikia Sera na Sheria tu. 

Alisema kuwa TAWA ailianzishwa mwaka 2016 Julai ambapo kazi kubwa ya Mamlaka ni kuhifadhi sehemu ya wanyamapori hayahifadhiwi na TANAPA na Ngorongoro "Hifadhi za Taifa ni maeneo ambayo yanaruhusu matumizi yasiyo ya uvunaji lakini maeneo mengine yaliyobaki ambayo ni Kilometa 230,000 yapo chini ya TAWA." Alisema Dkt. Wakibara. 

Aliongeza kuwa TAWA inamajukumu ya kusimamia wanyamapori ikiwa ni pamoja na kusimamia ustawi wao na kuona maisha yao yanakaa vizuri ,kuhakikisha rasilimali hiyo inatumika vizuri katika kukuza uchumi wa nchi. 

Pia alisema kuwa hali ya ujangili imepungua, mfano ujangili wa tembo umeshuka,ambapo mwaka 1982 wakati pori la Selous linaingizwa katika urithi wa dunia kulikuwa na tembo 100,oo6 lakini hivi karibuni tembo hawa walipungua mpaka kufikia 13,500 asilimia 87% ya tembo ilipotea.

Mfano katika hifadhi ya taifa ya Tarangire kipindi cha miaka miwili au mitatu hajapigwa tembo hata mmoja kwa ujangili, na hifadhi ya selous ndani ya miezi sita ya mwaka huu wa fedha hajapihwa tembo hata mmoja, na katika miaka miwili au mitatu kulikuwa na upotevu wa Tembo 17 mwa mwaka.

"Kiwango cha ujangili kimeshuka,na hata tumeanza kupokea maoni kutoka jumuia za kimataifa kutupongeza kwamba kwa kuwa imefanyika kazi kubwa kupambana na ujangili" alisema Dkt. wakibara .

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini