Tazama Picha : KINACHOENDELEA KWENYE MSIBA WA RUGE MUTAHABA BUKOBA

Mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds, Ruge Mutahaba yatahudhuriwa na vigogo zaidi ya kumi wakiwemo Mawaziri, Wabunge na Wakuu wa Mikoa.

Ratiba iliyotolewa leo asubuhi Jumatatu Februari 4,2019 inawataja baadhi ya vigogo hao ambao ni mawaziri na wizara zao kwenye mabano ni Dk Hamisi Kigwangalla (Maliasili na Utalii), Dotto Biteko (nishati), January Makamba (Muungano mazingira), Angela Kairuki(uwekezaji) na Juma Aweso ambaye ni Naibu Waziri wa Maji.

Pia, wabunge wanaotajwa kwenye ratiba hiyo ni Nape Nnauye (Mtama-CCM), Rudhiwani Kikwete (Chalinze-CCM), Aieshi Hilary (Sumbawanga Mjini- CCM) na wabunge wote wa Mkoa wa Kagera na wakuu wa wilaya.

Pia, yatahudhuriwa na Wakuu wa mikoa ya Simiyu (Anthony Mtaka), Mwanza (John Mongella), Mara (Adam Malima) na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Oseah Ndagala.
Waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko akiwasili katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi hii katika ibada ya kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba .
Mkuu wa Mkoa Mara, Mhe. Adam Malima akiwasili kwenye viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi ya leo kuhudhuria ibada ya mazishi ya aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba inayofanyika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba.
Hali ilivyo katika viwanja vya Gymkhana ndani ya manispaa ya Bukoba, ambapo viongozi mbalimbali, wananchi na wasanii wamejitokeza kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba.

Mbunge wa jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akimpa pole mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi hii katika ibada ya kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba.
Mbunge wa jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akisalimiana na mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zitto Kabwe baada ya kuwasili katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi hii kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba.
Mbunge wa jimbo la Sumbawanga mjini, Mhe. Aeshi Hillary akisalimiana na mbunge wa jimbo la Kigoma mjini, Mhe Zitto Kabwe katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba asubuhi hii katika ibada ya kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi Clouds Media Group marehemu Ruge Mutahaba.


Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini