Ujumbe wa mwisho wa rubani kwa mama yake | ZamotoHabari.

jumbe wa mwisho wa rubani kwa mama yake
Narudi nyumbani Nairobi, nimeshau simu yangu hotelini, tutaongea zaidi nikifika huko”.

Haya ni maneno ya mwisho ya Yared Tessema Getachew, rubani kijana aliyekuwa akirusha ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, iliyopata ajali mwishoni mwa wiki iliyopita na kuua watu 157 waliokuwemo


Maneno hayo alimwambia mama yake mzazi kwa kumtumia ujumbe wa simu, kabla ya kurusha ndege hiyo ya Boeing 737 Max 8, asubuhi ya Jumapili ya Machi 10, 2019.

Yared mwenye miaka 29 alikuwa ni raia wa Kenya, ndiye aliyekuwa rubani mkuu kwenye ndege hiyo iliyosababisha vifo vya mamia ya watu.

Mpaka sasa mwili wa rubani huyo bado haujapatikana, ili kufanyiwa mazishi kwa imani yake ya dini ya kiislam.

Baba wa rubani huyo Dr. Getachew Tesema,  amesema mtoto wake alikuwa mwenye akili sana darasani na alikuwa akipenda kuogelea, mpaka marafiki zake walimpa jina la 'Mr. Fish'.

Akiendelea kuelezea machungu yake, Dr. Tesema ameweka wazi kuwa kijana wake huyo mtanashati alikuwa ameshachumbia, na mipango ya ndoa ilikwishaanza.

Baba asimulia
“Alikuwa mchapa kazi na akimuheshimu kila mmoja, mkubwa au mdogo, watu walimpenda sana na kumuheshimu pia, alikuwa ni baraka kwa mambo mengi, na alikuwa karibu sana nami, nilimshawishi aende Ethiopia kwa masomo badala ya Afrika Kusini na kupata kazi kwenye shirika kubwa kama lile, nikatarajia ataleta mabadiliko makubwa sana, sioni kama kuna mtoto ambaye anaweza chukua nafasi yake, alikuwa wa kipekee”, amesema Dr. Tesema.

Akiwa mtoto wa 5 kati ya watoto 6 wa Dr. Tesema, Yared alizaliwa mwaka 1989 nchini Kenya, na mama yake ambaye pia ni daktari.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini