Wafanyakazi wa JKCI wamuaga Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto | ZamotoHabari

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney (kulia) baada ya kukamilisha muda wake wa kubadilishana uzoefu na wauguzi wa taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Bi. Mollie amefanya kazi katika chumba cha ICU katika taasisi ya JKCI kwa miezi 8
 Mkuu wa Kitengo cha ubora wa huduma za afya ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Tulizo Shemu akimpongeza Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney (kulia) kwa kushirikishana uzoefu na wauguzi wa JKCI wakati wa hafla fupi ya kumuaga. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi na wapili kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi ya JKCI Robert Mallya
 Baadhi ya wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney (hayupo pichani) baada ya kubadilishana uzoefu na wauguzi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi 8 na kuagwa  leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akimkabidhi zawadi ya fremu ya kuweka picha Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam baada ya kubadilishana uzoefu na wauguzi wa JKCI kwa kipindi cha miezi 8. Kulia ni afisa uuguzi mwandamizi wa taasisi hiyo Mary Haule
 Afisa Uuguzi Mwandamizi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mary Haule akimwekea zawadi ya gauni juu ya mwili wake Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam baada ya kubadilishana uzoefu na wauguzi wa JKCI kwa kipindi cha miezi 8.
 Afisa Uuguzi Mwandamizi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mary Haule akimfunga zawadi ya kikoi Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam baada ya kubadilishana uzoefu na wauguzi wa JKCI kwa kipindi cha miezi 8.
Afisa Uuguzi Mwandamizi mwenye utaalamu wa kuwahudumia watoto waliopo katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Marekani Mollie Mullaney katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari na wauguzi wa JKCI baada ya hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Bi Mollie Mullaney amefanya kazi katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum katika taasisi ya JKCI kwa kipindi cha miezi 8 na kubadilishana ujuzi na uzoefu na wauguzi wa ICI wa taasisi hiyo. Picha na: Genofeva Matemu - JKCI

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini