Wakenya Wadai Kuchoshwa na Ahadi za bure katika vita dhidi ya rushwa Kenya | ZamotoHabari.

Wakenya Wadai Kuchoshwa na Ahadi za bure katika vita dhidi ya rushwa Kenya
Kumekuwa na kilio cha umma nchini Kenya kufuatia ripoti kwamba mabilioni ya fedha yalionuiwa kufadhili mradi wa bwawa la maji katika eneo la Bonde la ufa magharibi mwa Kenya zimetuhumiwa kufujwa.

Hii ikiwa ni kashfa ya hivi punde kando na nyingine ambazo zimeshuhudiwa katika kpindi cha siku za nyuma ambazo hadi hii leo hazijatatuliwa.

Wakenya wamejitosa katika mitandao ya kijamii kuelezea hasira na kuchoshwa kwa kile wanachotaja kuwa ni vitisho vya bure kwa viongozi wafisadi katika serikali.

Moto unawaka Mlima Kenya
Marekani yatangaza $1m kwa mwanawe Bin Laden
Kifafa: Ugonjwa wa ajabu wa Afrika Mashariki
Netanyahu kushtakiwa kwa rushwa?
Baadhi wamekuwa wakieleza kwamba wanahisi Rais hajachukua hatua stahiki na kwa muda mrefu kufikia sasa amewaendekeza 'wahalifu' katika serikali.

Kwa kutumia #MrPresidentTumechoka raia wameelezea kuchoshwa kwao na matukio ya ufisadi Kenya.

Rais Uhuru Kenyatta mwenyewe amekiri hivi karibuni kwamba umma unazidi kuudhika kutokana na kukithiri kwa visa hivyo vya rushwa.

Ni nani wa kuwajibika?
Rais Uhuru Kenyatta ameeleza kwamba watuhumiwa wa ufisadi watachukuliwa hatua.

'Tuungane pamoja na tuseme ya kwamba tutapambana na tutapiga vita ufisadi tukiwa kitu kimoja.

Kwasababu hatuna njia nyingine, Wakenya wanahitaji barabara mahosiptali, stima, vijana wetu wanataka kazi, mambo haya hatutayapata tukifuata mwenendo ambao upo hivi sasa - 'Get rich quick' - hiyo haiwezi kutufikisha mahali ambapo taifa tunataka kwenda' ameeleza rais Uhuru Kenyatta hivi maajuzi akizungumza katika mazishi aliyoyahudhuria huko Muranga Kenya ya kati.

Mnamo 2015, rais Uhuru alitangaza rasmi vita dhidi ya ufisadi kama tishio kwa usalama wa taifa ambalo lilikuwa likipindukia.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini