Wanamgambo walijificha kwenye majengo Mogadishu | ZamotoHabari.

Wanamgambo walijificha kwenye majengo Mogadishu
Vikosi vya usalama nchini Somalia vinapambana na watu waliokua na silaha waliokuwa wamejificha kwenye jengo mjini Mogadishu, saa kadhaa baada ya shambulio la kujitoa muhanga lililotekelezwa kwenye gari katika eneo la mtaa uliokuwa na pilikapilika na kusababisha vifo vya watu takriban saba.

Shambuli hilo lilitokea siku ya Alhamisi lililotekelezwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa al-Shabab katika eneo lililokuwa na hoteli, maduka na migahawa.

Watu waliokuwa na silaha baadae walizungukwa na vikosi vya usalama

Majibizano ya risasi yaliendelea usiku mzima mjini Mogadishu.


Shambulio lilitokea eneo lenye hoteli na migahawa
Watu takribani 60 wamejeruhiwa na saba wamepoteza maisha, msemaji wa huduma ya gari za kubeba wagonjwa aliiambia BBC.

Watu kadhaa waliokolewa kutoka ndani ya jengo hilo, ripoti zimeeleza.Kuna wasiwasi kuwa idadi ya wanaoelezwa kupoteza maisha huenda ikaongezeka.

''Bado kuna watu wenye silaha ndani ya jengo,'' Afisa wa polisi Ibrahim Mohamed alinukuliwa siku ya Ijumaa asubuhi na shirika la habari la Ufaransa, AFP

Katibu mkuu wa umoja wa waandishi wa habari wa Somalia Mohamed Moalimuu alikuwa ndani ya Hoteli ya Maka al-Mukarama akiwa na mwezie waliposikia milio ya risasi ikifuatiwa na mlipuko.





Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini