Waziri awacharukia Wakala wa chakula | ZamotoHabari.

Waziri wa kilimo Japhet Hasunga ametishia kufuta wakala wa hifadhi ya chakula nchini (NFRA), iwapo hautakuwa na uwezo wa kununua zaidi ya tani laki tano za mazao kila msimu kutoka kwa wakulima na kuyatafutia masoko ndani na nje ya nchi.
.

Akizungumza katika uzinduzi wa mtambo wa kusafisha mahindi uliotolewa na mpango wa chakula duniani (WFP), kwa NFRA, Mh. Hasunga amesema kazi ya wakala huo sio kuhifadhi tu chakula bali lazima wanunue mazao yote ya ziada kwa wananchi na kuyatafutia masoko.

Mh. Hasunga akizungumzia mtambo huo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 399 amewataka watendaji wa NFRA kuhakikisha wanautunza na kuufanyia matengenezo mara kwa mara.

Awali kaimu mtendaji wa NFRA Vumilia Zikankuba amesema wakala huo umekuwa ukishirikiana na WFP kwa muda mrefu katika kuboresha miundombinu na teknolojia za kuhifadhi chakula huku zoezi la kuuza tani 36,000 likiendelea.

Aidha ameeleza kuwa hadi sasa wameshauza zaidi ya tani 20,400 huku mwakilishi mkazi WFP akisema wametoa dola za kimarekani milioni 300 tangu mwaka 2010.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini