Waziri Jafo atoa agizo kwa Wakuu wa Mikoa | ZamotoHabari.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jaffo amewaagiza Wakuu wa Mikoa  na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote nchini kuwawezesha Maafisa Utamaduni kwa kuwaongezea Bajeti itakayowawezesha kutimiza majukumu yao kwa ufasaha.

Agizo hilo amelitoa leo Jijini Dodoma wakati alipokuwa akifunga Kikao Kazi  cha  11 cha Maafisa Utamaduni kilichofanyika kwa siku mbili ambapo amewaagiza Wakurugenzi kutambua majukumu ya maafisa Utamaduni  ikiwemo kuhifadhi kuendeleza mila na desturi pamoja na kukuza lugha ya kiswahili.

"Sekta hii ni muhimu sana kwakua ina wajibu wa kuelimisha na kuburudisha,hivyo naendelea kuwasitiza Wakurugenzi kuwawezesha Maafisa Utamaduni kushiriki katika kila Mkutano,kongamano,warsha zote zinazohusu sekta hiyo,”Alisema Jaffo.

Aidha ameongeza kuwa thamani ya maafisa Utamaduni ni lazima ionekane kwakua ndio tasnia inayofundisha na kukuza Uzalendo hasa kujua alama,nyimbo na tunu za Taifa kwa vijana na wanafunzi nchini.

Katika hatua nyingine, Jaffo amewahakikishia Maafisa Utamaduni kuwa wavumilivu kuhusu muundo wa Kada hiyo ambapo amewaahidi kuwa suala hilo limepokelewa na Serikali itaanza mchakato wake ili kutatua changamoto hiyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Susan  Mlawi amesema kuwa Kikao Kazi hicho ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 inayoeleza kuwa Wasimamizi na Watendaji wakuu wa shughuli za Utamaduni katika ngazi ya Taifa, Mkoa Wilaya na Taasisi za elimu na mafunzo kupata mafunzo ya uendeshaji ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini