Bondia Aliyefungiwa, Mpenzi Wake Amkingia Kifua | ZamotoHabari.

Bondia aliyefungiwa, mpenzi wake amkingia kifua
Baada ya Bondia Kubrat Pulev kufungiwa kucheza mchezo wa masumbwi baada ya tukio la kumpiga busu mwandishi wa habari aliyekuwa anamuhoji baada ya ushindi wa pambano lake na Bogdan Dinu, mchumba wake ameibuka na kumtetea kwakile alichokiita ni mbinu za kumuua mpenzi wake.

Mwanadada huyo anayejulikana kwa jina la Andrea, akifanya mahojiano na moja kati ya chombo cha habari nchini humo, ameoneshwa kutoridhishwa na adhabu aliyopewa mpenzi wake na kuiita kuwa ni uonevu dhidi ya Bondia huyo.

"Hii ni adhabu mbaya sana kwake, kwani haya ndiyo maisha yake. Mimi sijaona kama kilikuwa kitu kikubwa hivyo kumfanyia hivi ni kumuua", amesema Andrea.

Tume ya michezo ya mji wa Calfornia, Marekani imetangaza kumfungia kushiriki pambano lolote kwenye mji huo hadi pale atakapojitokeza na kufanya mazungumza nao kuhusiana na hilo tukio.

Jenny Sushe, ambaye ndiye mwandishi wa habari aliyefanyiwa kitendo hicho pia amemfungulia mashtaka mahakamani mwanamasumbwi huyo.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini