BONDIA ROJAS MASAMU AJIGAMBA KUMCHAKAZA MKWERA SIKU YA PASAKA | ZamotoHabari

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

BONDIA Rojas Masamu ametamba kumsambalatisha bondia Idd Mkwera katika raundi za awali kwa madai kuwa hataki kuwapa tabu majaji watakaosimamia pambano lao.

Masamu ameiambia Michuzi Blog leo Machi 3,2019 jijini Dar es Salaam kuwa kwa sasa yupo fiti na ana uchu wa kupambana huku akijagamba kumchakaza mpinzani wake Mkwera kwani kipigo atakachompa hatakisahau mpaka anaingia kaburini"Najiamini vya kutosha, nimefanya mazoezina hivyo nina kila sababu za kushinda tena mapema tu.Mkwera ajipange kwelikweli.

"Nipo kambini sasa yapata miezi miwili kwa ajili ya mpambano huu , hivyo asichukulie poa kabisa kwani kwa sasa nimeongeza dozi ya kufanya mazoez.Awali nilikuwa nafanya mazoezi mara mbili kwa siku lakini kwa sasa nafanya mara tatu kwa kuwa nataka kumpiga kwa K,O mbaya ambayo itawashangaza wapenzi na mashabiki wa mchezo wa ngumi,"amesema.

Kwa mujibu wa ratiba ya mpambano huo ambao umeandaliwa na Promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ni kwamba litafanyika Siku ya Sikukuu ya Pasaka na kwamba limepewa nguvu na bondia Mtanzania Omari Kimweri 'Lion Boy 'anayeefanya shughuli zake nchini Australia.

Super D amesema kuwa bondia huyo ndiye aliyesabababisha mabondia hao wawili kuwekewa pambano hilo kwani vijana wanatakiwa kuendeleza rekodi zao za masumbwi kila wakati.Ameongeza mbali ya pambano hilo pia siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine kadhaa.

Amesema kuwa bondia Hussein Pendeza atamkabili Juma Ramadhani 'Choki' na Shomari Milundi ataoneshana umwamba na Bakari Mbede wakati Ibrahimu Makubi atavaana na Haruna Ndalo wakati Ramadhani Mbegu 'Migwede' atakabiliana na Rashidi Mnyagatwa.

Pia bondia Salum Tandu atapambana na Gerald Mkude na Sunday Kiwale 'Moro Best' atavaana na Luckman Ramadhani wakati Vicent Mbilinyi atapambana, Shabani Mbogo na Hussein Shemdoe, Shehe Azizi na Ahmadi Kombo atapambana na Sandali Nyambala

Super D amesema mapambano yote hayo yamedhaminiwa na kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion ambayo ipo nchini Tanzania kwa ajili ya kuinuwa vipaji ya vijana mbalimbali ili kuendeleza vipaji vyao pendwa

na kwa kupitia kampuni ya Super D Promotion imejidhatiti kuweka angalau pambano moja kila baada ya miezi miwili ili kuwasaidia vijana kukuza vipaji vyao na kujiendeleza kupitia mchezo uho wa masumbwi nchini.


Bondia Ramadhani Mbegu 'kushoto' akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Idd Mkwera wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika siku ya pasaka April 21 katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu magomeni Mapipa Mbegu atacheza na Rashidi Mnyagatwa na Mkwera atapambana na Rojas Masamu 
Bondia Idd Mkwera 'kushoto' akioneshana umwamba wa kutupiana makonde naRamadhani Mbegu wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika siku ya pasaka April 21 katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu magomeni Mapipa Mbegu atacheza na Rashidi Mnyagatwa na Mkwera atapambana na Rojas Masamu 
Bondia Sunday Kiwale 'Moro Best' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Shehe Azizi wakati wa maoezi yao ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika siku ya Pasaka April 21 katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu Kiwale atapambana na Luckman Ramadhani na Azizi atapambana na Hussein Shemdoe


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini