Clouds Media wakanusha Mtangazaji wa Shilawadu Kuwekewa Sumu | ZamotoHabari.

Clouds Media wakanusha Mtangazaji wa Shilawadu kuwekewa Sum
Kituo cha Radio, Clouds FM kimekanusha taarifa zilizosambaa mtandaoni zikidai kuwa Mtangazaji
wao Soudy Brown amewekea sumu.

Taarifa iliyotolewa na Radio hiyo imesema Mtangazaji huyu yupo salama na hakuna chochote kibaya kilichompata.

"Kuna Taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kumuhusu mtangazaji na mfanyakazi wa Clouds Media Group Soudy Brown kuwa yupo mahututi amepewa sumu taarifa hizi si za kweli tunawaomba utulivu. Soudy yupo salama na amepumzika nyumbani kwake,"
alieleza taarifa hiyo.

Soudy Brown amekuwa maarufu zaidi hasa pale alipoaza kuonekana Clouds TV kupitia kipindi cha Shilawadu.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini