Rais Dkt John Magufuli ameendelea na ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Mtwara, ambapo anakagua na kuzindua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali mkoani humo.
Ambapo leo Aprili 3, Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi katika mradi wa barabara ya kutoka Mtwara Mwinyivata yenye urefu wa kilomita 50 ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya kutoka Mtwara, Tandahimba, Newala, Masasi yenye urefu wa kilomita 210.
‘‘Niwapongeze kituo cha Utafiti cha Naliendele, mnafanya kazi nzuri, nimeambiwa mnatengeneza utafiti wa kupata juisi kutoka kwenye korosho.
“Kama ni divai ya korosho au ni gongo ambayo ni ‘special’ itengenezeni iliyopimwa kwamba percentage ya alcohol ni kiasi fulani, hata hizi pombe kali zinazokuja si ni gongo tu, lakini zimepimwa. Sasa mtengeneze gongo ya aina yake ambayo ni nzuri, tunavidharau vitu vyetu,’’ amesma Rais Dkt. John Magufuli.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments