Kutotengwa rasilimali za kutosha kufikia Usawa wa Kijinsia ni Ndoto | ZamotoHabari

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Shirika la TGNP Mtandao limesema kuwa kutotengwa rasilimali za kutosha, kutolewa  na kutekelezwa kwa wakati itakuwa ndoto kufika usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu pamoja na ufanisi wa mikataba ya Kimataifa, sera na bajeti yenye mrengo wa kijinsia.

Hayo yameelezwa Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao Bi.Asseny Muro kwenye ufunguzi wa mdahalo kabla ya bajeti kuu ya Taifa ya mwaka 2019/2020 ambapo amesema TGNP imekuwa mstari wa mbele katika kutetea masuala ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji Wanawake.

Aidha ameongeza kuwa wakati TGNP ikitimiza miaka 25 tangu ianzishwe imekuwa na mikakati mingi ambayo imekuwa ikitumika katika kuleta maendeleo kwa jamii, hasa usawa wa kijinsia na haki ya jamii, uchambuzi wa sera, mipango na bajeti kwa mrengo wa kijinsia pamoja na mafanikio ya mabadiliko ya kimtazamo na kimaoni kwa Wanawake kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Utafiti na Uchambuzi wa sera na Bajeti kutoka TGNP Happiness Maluchu amesema mdahalo huo umehusisha wadau wa  makundi mbalimbali ikiwemo makundi maalumu na wachambuzi wa sera za kibajeti ili kuhakikisha kuwa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda watu waliopembezoni ikiwemo makundi maalumu na wale wa vijijini hawaachwi nyuma.

Hata hivyo amesema kuwa katika utekelezaji wa bajeti ambazo zimepita changamoto kubwa ipo kwenye ufikishwaji wa fedha kwa kiwango ambacho kimepangwa kwenye utekeleza wa mipango iliyowekwa hivyo kukwamisha ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
 Mkuu wa Idara ya Utafiti na Uchambuzi wa Sera na Bajeti Happiness Maluchu akizunguma katika warsha ya kujadili Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwa kuangalia usawa wa kijinsia lililofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mwanaharakati Janeth Mawinza akizungumza kuhusiana na wanawake kutoshirikishwa katika mipango mbalimbali ya serikali katika warsha ya TGNP iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau mbalimbali katika warsha ya TGNP

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini