Lema na Halima Mdee Wakutana na Rungu Bungeni | ZamotoHabari.

Wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) GodlesLema ambaye ni Mbunge wa Arusha mjini pamoja na Mbunge wa jimbo la Kawe Jijini Dar Es Salaam Halima Mdee leo hii katika kikao cha Bunge jijini Dodoma wamejikuta wakikumbana na rungu la Bunge kwa kupewa baadhi ya adhabu.


Chini ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson ameagiza Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kutamka bungeni kuwa Bunge ni dhaifu.


Lakini pia kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imependekeza Bunge kumsimamisha mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kuhudhuria mikutano miwili ya Bunge kuanzia tarehe ya azimio hilo kutokana na kuunga mkono kauli ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuwa Bunge ni dhaifu. Mdee alihojiwa na kamati hiyo kwa kauli hiyo.


Mbali na hilo Wabunge wa upinzani wametoka nje ya Ukumbi wa Bunge wakipinga maamuzi yaliyochukuliwa dhidi ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee. Mdee amepewa adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili ya Bunge kwa kuunga mkono kauli ya CAG kuwa Bunge ni dhaifu.


Na baada ya yote Bunge likapitisha azimio la kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini