MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema atakutana na kina mama wajane, jijini Dar es Salaam, Aprili, 4, mwaka huu, ili kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili, likiwemo suala la mirathi na kutoa elimu kwao kuhusu fedha ambazo ni asilimia nne zinazotengwa kila manispaa kwa wanawake ili wajue kuwa fedha hizo zinawahusu.
Makonda ameyasema hayo ofisini kwake leo akiongea na waandishi wa habari.
Pia amepongeza wakuu wa wilaya za Ilala na Temeke kwa kukamilisha zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo-wadogo kwenye maeneo yao, na amewataka wakuu wa wilaya za Kigamboni, Kinondoni na Ubungo kuongeza kasi ya kukamilisha zoezi hilo.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments