Matumaini Mapya Mkutano wa Tatu Kati ya Trump na Kim | ZamotoHabari.

Matumaini Mapya Mkutano wa Tatu Kati ya Trump na Kim
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo, ameelezea matumaini kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na Rais Donald Trump watakutana tena katika miezi ijayo, na kufikia muafaka juu ya kukomesha mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Katika mahojiano yaliotangazwa leo, Pompeo alitahadharisha kuwa ni vigumu kujua wakati wa mkutano wa tatu wa kilele kati ya Marekani na Korea Kaskazini, lakini amesema ni katika maslahi ya Marekani kutatua suala hilo haraka iwezekanavyo.

 Trump na Kim walikutana kwa mara ya kwanza Juni 2018, katika mkutano wa kihistoria ambao haukuvimaliza rasmi vita vya Korea vya mwaka 1950 hadi 53.

Mkutano wa pili mwezi Februari mjini Hanoi, ulivunjika mapema ghafla baada ya wawili hao kushidwa kuafikiana kuhusu kuondoa vikwazo, lakini Trump amesema bado anampenda kiongozi huyo wa Korea Kaskazini, na hivi karibuni aliingialia kati kuzuwia nchi hiyo kuwekewa vikwazo vikali zaidi.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini