Mbowe Afunguka Kuhusu Adhabu ya CAG Bungeni | ZamotoHabari.

Mbowe afunguka kuhusu adhabu ya CAG Bungeni
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema azimio la Bunge la kutokuwa tayari kufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) litalihukumu Bunge.

Leo Kamati ya Maadili Haki na Madaraka ya Bunge imemtia hatiani Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kwa kulidharau bunge. Kufuatia hatua hiyo Kamati imetoa mapendekezo ya Bunge kutofanya kazi na CAG, Prof. Asaad.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maadili, Emmanuel Mwakasaka amesema kamati imemtia hatiani CAG, Profesa Mussa Assad kuhusu kauli yake ya 'udhaifu wa Bunge' aliyoitoa wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini