Mchekeshaji Pierre Konki Liquid, ametembelea Bungeni jijini Dodoma baada ya kupata mwaliko kutoka kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Akizungumza na wanahabari baada ya kutoka ndani ya Bunge, amemshukuru Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa kumpa ofa ya tiketi kwa ajili ya kwenda nchini Misri kuhamasisha mashabiki wa Timu ya Taifa katika michuano ya AFCON mwaka huu.
Pierre amefungukia pia ishu iliyosambaa mwanzoni mwa wiki hii baada ya RC Paul Makonda kuwataka wanahabari kuwapa nafasi watu wanaoisaidia jamii badala ya watu ‘walevi’ na ‘wa hovyo’ kama Pierre.
Pierre amepata umaarufu mkubwa baada ya kusambaa kwa video zake mitandaoni akiwa amelewa huku akitamka maneno kama ‘Mama nakufa’ na kufanya vituko ambavyo vimependwa na watu haki kumpelekea kupata ubalozi katika makampuni mbalimbali.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments