Rais wa Algeria Bouteflika atangaza kujiuzulu

Rais wa Algeria Bouteflika (82) ambae anatumia wheelchair kutembelea amejiuzulu wadhifa wake baada ya kukaa madarakani kwa miaka 20, hatua hiyo inakuja baada ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Algeria Ahmed Gaid Salah kumtaka Rais huyo ajiuzulu haraka iwezekanavyo.

Kulikuwa na shangwe na vifijo kwenye mji mkuu Algiers baada ya kutangazwa uamuzi huo jana usiku. Televisheni ya taifa ilitangaza kuwa Bouteflika alilishauri rasmi Baraza la Katiba kuwa anaachia madaraka kama Rais wa Algeria. 

Alisema uamuzi huo uliochukuliwa kwa dhati unalenga kuchangia katika kuituliza mioyo na fikra za Waalgeria, na kuwawezesha kuiongoza Algeria kuwa na mustakabali mzuri na ambao wana haki ya kuufanikisha. 

Video ilimuonyesha Bouteflika, akiwa kwenye kiti cha walemavu, akikabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa mkuu wa Baraza la Kikatiba Tayeb Belaiz.



Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini