Rais wa China Aililia New Zealand Kuhusu Huwawei | ZamotoHabari.

Rais wa China aililia New Zealand kuhusu Huwawei
Rais wa China Xi Jinping ameitaka New Zealand leo kutobagua makampuni ya China wakati alipokutana na waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern, ambaye nchi yake ilikataa ombi la kampuni la China la masuala ya mawasiliano Huawei kujenga mtandao wa simu za mkononi wa 5G.

Ardern, akiwa katika ziara ya siku moja nchini China, alisema kabla ya mkutano na Xi kwamba ana matumaini ya kuwa na majadiliano na serikali ya China juu ya uamuzi wa shirika la New Zealand la intelijensia kukataa ombi hilo.

Mahusiano na China yameingia katika hali ya wasi wasi chini ya serikali ya Ardern ambayo imeonesha wazi wasi wasi wake juu ya kuongezeka kwa ushawishi wa China katika eneo la kusini mwa bahari ya Pasifiki. Wakikutana mjini Beijing Xi alimwambia Ardern kwamba China imekuwa wakati wote ikiiangalia New Zealand kama rafiki na mshirika mwaminifu.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini