WAZIRI MKUU MGENI RASMI MBIO ZA SOKOINE MARATHON ,WANANCHI WAJIANDIKISHA MCHANA NA USIKU KUSHIRIKI | ZamotoHabari

Na Woinde Shizza Globu ya jamii.


Zoezi la uandikishwaji wa mbio za kumuenzi hayati Edward Sokoine linafanyika usiku na mchana ili kutoa nafasi kwa wale waokuwa kazini wakati wa mchana ili wapate nafasi ya kujiandikisha kushiriki mbio hizo.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Lembrisi Kipuyo aliyasema hayo Leo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mwisho ya mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika April 6 jijini Arusha.

Akizungumzia swala la uandikishwaji usiku na mchana alisema awali walikuwa wanaandikishwa mchana lakini kutokana na maombi ya watu wengi kuchelewa makazini ndio maana wameamua kuandikisha adi usiku wa SAA mbili.

Alisema uandikishwaji umeanza tangu wiki iliopita katika vituo viwili ambavyo ni uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini hapa pamoja na ofisi za utamaduni na michezo wilayani Monduli huku akibainisha kuwa muitikio wawashiriki wa mbio hizo ni mkubwa.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha riadha mkoani Arusha Alfred Shahanga alisema kuwa njia zimeshapimwa na kuthibitishwa na njia za mbio hizo zitakuwa katikati ya jiji la Arusha na kwaupande wa swala la usalama ni la uhakika.

"Mbio zote zitaanzia mnara wa saa na zitamalizikia katika uwanja wa sheik Amri Abeid na mgeni rasmi wa mbio hizo atakuwa Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa Kasimu " alisema Shahanga

Alitaja zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa kilometa 21 kuwa mshindi wa kwanza atapatiwa kiasi cha shilingi milioni moja ,mshindi wa pili shilingi laki saba na mshindi wa tatu atapatiwa laki tano.

Shahanga aliwataka wakazi wa Mkoa wa Arusha na Mkoa Jirani kujitokeza kushiriki mbio hizo ili kuenzi kwa pamoja kuanzimisha miaka 38 ya kifo cha aliekuwa Waziri mkuu wa zamani hayati Edward Moringe Sokoine.


Picha Mwenyekiti wa Sokoine Marathon Lebris kipuyo akiongea na waandishi wa habari


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini