YANGA INAENDELEA KUMKOSA AJIB MCHEZO WA KESHO DHIDI YA NDANDA FC | ZamotoHabari

KIKOSI cha Yanga kinatarajia kushuka kesho kuwavaa Ndanda Fc katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona  ikiwa ni muendelezo wa mchezo ligi kuu soka Tanzania bara (TPL).

Yanga wataendelea kukosa huduma ya nahodha wao  Ibrahimu Ajib akisalia Dar es Salaam akiendelea kupata matibabu.

Imeripotiwa kuwa Nahonda wa kikosi cha Yanga Ibrahim Ajibu hajasafiri na na timu yake na hatakuwa katika sehemu ya  mchezoni siku hiyo, ikiwa ni mchezo wa pili mfululizo  kukosa kucheza, mwingine ambao aliukosa ni mechi ya  robo fainali kombe la FA dhidi ya Alliance fc kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza mwishoni mwa wiki.

Aidha Afisa habari wa Yanga, Dismas Ten ameiambia Yanga Tv kuwa "Nahodha Ibrahim Ajib ataendelea kukosekana kikosini kutokana na majeraha hivyo hatakuwa katika sehemu ya mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Nangwanda sijaona ambapo kikosi chetu kitavaana na Ndanda Fc"

Hata hivyo mchezaji huyo amesema  kuwa  kukosekana kwake kikosini na kukosa mchezo wa pili mfululizo  kunatokana na maumivu ya nyonga ambayo yamekuwa yakimsumbua siku za hivi karibuni

Vilevile kufuatia sakata hilo la Ajib kutosafiri na timu yake  katika mechi hizo baadhi ya magazeti yameripoti kuwa Ajib tayari amemalizana na mabosi wa Simba ambao wamemtengea mkataba wa miaka miwili

kutokana na taarifa zinazotawala katika vyombo vya habari kuwa yuko mbioni kurejea Simba, Ajib amenukuliwa gazeti la mwanasport akisema "ukweli au uongo wa taarifa hizo utafahamika msimu ukimalizika mimi nina mkataba na klabu ya Yanga, nitaendelea kuitumikia timu yangu.”

Mchezaji huyo ameendelea kusema kuwa  "hizo taarifa za mimi kusajiliwa na Simba ukweli au uongo wake utafahamika mwishoni mwa msimu, Mimi ni mchezaji wa Yanga ni vyema nikaulizwa mambo yanayoihusu Yanga, hayo mengine tuwaachie wanaotumia kalamu zao kujinufaisha kwa kuuza magazeti lakini ifahamike mimi ni mchezaji wa Yanga"

Pia  hivi karibuni kaka yake Athumani Ajib ambaye ndiye wakala wake, alikanusha taarifa hizo huku akibainisha kuwa wamefanya mazungumzo ya mkataba mpya na Yanga lakini wamekubaliana ni vyema wakasubiri mpaka mwishoni mwa msimu ndio aweze kusaini mkataba mpya.

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini