BABUTALE AFICHUA SIRI YA MAFANIKIO YA WASAFI, DINI HAINA NAFASI | ZamotoHabari

Na Khadija Seif, Globu ya jamii

MENEJA wa msanii Diamond platinum  Khamis Tale Tale a.k.a Babu Tale amempongeza msanii Harmonize kwa alipofikia. Aidha, tale amesema harmonize alikua msanii wa kwanza kusainiwa katika kundi hilo .

"Alikuja wasafi hajui Kiingereza kutokana na kutengenezwa na kuwa msanii wa kimataifa ilimlazimu ajifunze kingereza kuwafikia mashabiki wa kila Kona ya afrika,"

Hata hivyo tale amesema harmonize ni msanii ambae anatambulika vizuri na muziki wake unapendwa na wengi kutokana na nidhamu yake ya kazi na kukipigania kile anachokifanya.

Pia ameweka wazi  sababu zinazofanya wasanii wa kundi hilo rayvan,lavalava,queen darling,mboso , harmonize pamoja na diamond platinum kufanikiwa na kipeperusha bendera nchi zingine ni kutokana na viongozi wa kundi hilo kuwalea kwenye misingi mizuri.

"WCB ni kundi ambalo maadili, nidhamu, upendo na uchapakazi ni miongoni mwa vitu vinavyopewa kipaumbele sana, hivyo Swala la kabila na dini halina nafasi katika kundi la wasafi japo msanii rayvan peke yake ndio dini nyingine lakini kutokana na viongozi wanawalea kwa usawa imekua ngumu kuona utofauti miongoni mwao"

Pia ametoa rai kwa wasanii wengine na makundi mengine kuwa na uvumilivu,b usara na hekima kwa sababu licha ya kundi la wasafi kupitia changamoto za kibiashara kuanzia kutopigwa kwa nyimbo zao kwa baadhi ya vyombo vya habari lakini waliweza kusimama na kuamini ipo siku watasonga mbele.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini