KOCHA wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa kesho watapambana kupata matokeo mbele ya Simba uwanja wa Uhuru.
Coastal Union wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga kwa kufungwa jumla ya mabao 2-1.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mgunda amesema kuwa amejipanga kulipa kisasi kwa Simba kutokana na ushindani uliopo kwa sasa kwenye ligi ana imani ya kupata matokeo.
"Simba ni timu kubwa nimecheza nao mchezo uliopita wamenipa taabu ila hilo halitajirudia tena safari hii nipo tayari kupata matokeo.
"Safu yao ya ushambuliaji yenye kasi naitambua hivyo inanifanya nije na mpango mpya wa kubadili mbinu zao na kubadili mfumo, kila kitu kinawezekana wakati wetu wa kushinda ni sasa, mashabiki watupe sapoti," amesema Mgunda.
Coastal Union imecheza jumla ya michezo 33 ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 41, Simba ipo nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 30 ina pointi 78.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments