Wanawake kuchagua wanaume masharobaro aka badboys kuwaliko wanaume wa kawaida si jambo geni na hutokea mara kwa mara. -aidha katika vyuo, vilabuni, sinema, maktabani ama sehemu yeyote ile. Wanaume masharobaro, kama wanaume wengine, wao pia wanamaumbo ya kila aina, shepu na mvutio wa kijinsia. Kama wewe ni mwanamume wa kawaida ambaye humaliza wa mwisho ama ushawahi kupoteza mpenzi wako kwa sharobaro fulani, hapo chini kuna nadharia ambazo zitasaidia kueleza kwa nini wanawake wanapenda sana kuvutiwa na wanaume masharobaro.
1. Hamu ya kufuata
Kufuata kitu ambacho unakipenda huwa kuna msisimko fulani mtu hupata. Lakini msisimko zaidi hutokea wakati ambapo mtu anajaribu kufuata mtu ambaye hataki kujulikana mienendo yake ya kimaisha, kufuatwa ama kueleweka kimaisha. Haya ndio maisha anayoishi mwanamume sharobaro. Wanawake wanapenda sana wanaume ambao hawaeleweki kimaisha (yaani hawatambuliki) ama kutaka kujua maisha yao. Na wewe kama mwanamume unataka kutumia huu udhaifu kwa manufaa yako, wakati mwingine unafaa kumfanya mwanamke abaki na maswali chungu nzima kutaka kukujua zaidi. Kama unampenda, jaribu kadri iwezavyo kutojaribu kumuonyesha. Badala yake mpe pia yeye changa moto kwa kuweka ujanja wa kutoeleweka mara kwa mara. Hii ni njia moja murua ya kuhakikisha utaingia katika akili yake.
2. Kutaka kuwafunga fundo
Kitu kingine ambacho wanawake huvutiwa kwa sharobaro ni kutaka nafasi ya kuwafunga fundo ama kuwajeuza tabia zao. Mwanamke, amezaliwa naturally na hisia za uzazi, yaani kutaka kujeuza mtu mwenye tabia ovyo kuwa na tabia nzuri. Hii huibua hisia halizi za uzazi ndio maana kama mwanamume unapaswa wakati mwingine kumsumbua mwanamke hikisia, kimawazo na kadhalika. Unafaa kuwa mpinzani lakini usiwe mhalifu. Unafaa kuwa hatari lakini usipitishe kiwango ambacho kitamwogopesha. Kimtazamo, unafaa kumfanya mwanamke auonyeshe uke wake wote ili kujaribu kukubadilisha, mpe nafasi ajaribu kuubadilisha upande wako wa kiza na mwishowe kukufanya uwe mwanamume thabiti katika mchakato mzima.
3.Uanaume uliothabiti
Wanaume masharobaro (na si wale feki) karibu nyakati zote huwashinda wanaume wa kawaida kwa sababu ya mambo mawili makuu. Kwanza ni kuwa ni wanaume majasiri na pili wanaudhibiti uanaume wao kwa kuwa ngangari kimaisha. Kutoogopa kwao kwa jambo lolote ndiko kunawafanya wanawake kuvutiwa nao. Wanawake wengi wanavutiwa na wanaume ambao ni hatari, ngangari na wenye nguvu kwa sababu si rahisi kuchezewa au kufanyiwa masihara. Ukismama kumtetea mwanamke kuhusu mahitaji yake na uovu, hii inamaana ya kuwa una uwezo wa kusimama kando yake na jambo lolote lile. Kuweza kuonyesha level ya kuwa wewe ni mtu usiekuwa na woga wowote, unafaa kumwonyesha mwanamke wako kuwa una uwezo wa kuwa ngangari mahali popote pale ili mradi kumlinda yeye tu.
4. Uoga wa kujitwika majukumu
Wanaume masharobaro hupenda kuhepa majukumu yanayohusiana na mahusiano. Kwa wanawake ambao wana uoga huo huo wa kuwa na majukumu, masharobaro huwavutia sana na kuwaona kama hakuna wanaume wazuri kama hao. Kwa kuwa wanawake hawatajitweka majukumu, huwa hawana haja ya kujishughulisha na hisia za kipenzi ambazo ni stress. Pia ni habari njema kwa wanawake ambao wako tayari kwa uhusiano wa kimapenzi wa muda mfupi pekee. Lakini kama kawaida, mwisho wa siku lazima mwanamume sharobaro au mwanamke mtundu lazima kuna sehemu fulani ndani ya mawazo yake anatamani kuwa na mahusiano ya kudumu na pia kupendwa. Hivyo siri hapa ni kuipima miondoko yake na uangalie level yake ya kujitwika majukumu katika mapenzi halafu sasa uanze na hapo.
Upende usipende, wanaume masharobaro watakuwa na nafasi kubwa katika moyo wa mwanamke. Kuna kitu ndani yao ambacho kinawasababisha wanawake kuangua mwili mzima kihisia na kimapenzi kwao. Lakini hii haimaanishi kuwa lazima kila mwanamume ajeuke na kuwa sharobaro ili aweze kuwa na nafasi rahisi ya kutongoza mwanamke aliye kwa ndoto zako. Kile unachotakiwa kufanya ni kucheza mchezo mzima kiwastani. Daima unafaa kuwa vile ulivyo huku ukiingiza tabia flani za usharobaro hivi katika miondoko yako. Kama kuna kitu nzuri kati yenu wawili, basi pia kuna sehemu mbaya ambayo unaweza kuitumia ili ukajinufaisha nayo
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments