MBUNGE MAVUNDE ASHIRIKI NA WANANCHI UJENZI WA ZAHANATI, ACHANGIA SARUJI MIFUKO 100 | ZamotoHabari.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde ameshiriki katika hatua za awali za ujenzi wa Zahanati ya Mtaa wa Msembeta, Kata ya Chigongwe Jijini Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake kwa wananchi hao aliyoitoa Tarehe 6.04.2019 wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi ambapo hoja ya ukosefu zahanati ilijitokeza na Mbunge Mavunde akaahidi kuanzisha ujenzi wake.

Mbunge Mavunde pamoja na kuchimba msingi wa zahanati hiyo akishirikiana na wananchi pia amekabidhi mifuko ya Saruji 100 na kuahidi kusimamia kukamilika kwa zahanati hiyo na kuondoa adha ya wakazi 2300 ambao wanatembea kilomita 10 kufuata huduma za Afya.

Akishukuru kwa niaba ya wananchi, Bi. Esther Masimami amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuanzisha mchakato huo wa ujenzi ambao utawapunguzia adha kubwa ya ukosefu huduma ya Afya kwa wakati na kuahidi kujitolea katika nguvukazi kama sehemu ya mchango wao kwenye zoezi la ujenzi.
 Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akizungumza na wananchi wa mtaa wa Msebweta mapema kabla ya Kushiriki zoezi la Uchimbaji Msingi.
 Baadi ya Wananchi wa Msebeta wakiendelea wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde alipofika Kijijini hapo kutimiza ahadi yake.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akishiriki kwa vitendo zoezi la uchimbaji wa msingi tayari kwa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji

 Mifuko 100 ya saruji iliyokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kama ahadi yake katika Ujenzi wa Zahanati ya Msembeta ili kuboresha utoaji wa huduma ya Afya.



Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini