Msimu wa pili wa MultiChoice Talent Factory Wafunguliwa | ZamotoHabari.

• Vijana wenye kiu ya kuwa wabobezi wa filamu kupata udhamini
• Mafunzo ya kitaalamu ya mwaka mzima kutolewa
• Ni kwa udhamini wa MultiChoice
Mpango wa umoja wa Afrika unatafuta wabunifu 60 wa filamu na televisheni barani kote Afrika kuwa sehemu ya darasa la mwaka 2019.

Vijana 60 kutoka kote barani Afrika – ikiwemo Tanzannia watapata fursa ya udhamini wa kujifunza uzalishaji wa filamu na vipindi vya televisheni kwa mwaka mzima katika  awamu ya pili ya program ya MultiChoice Talent Factory

Kuanzia tarehe 7 Mei 2019 hadi tarehe 14 Juni 2019, vijana wenye uchu wa kuwa wabobezi wa filamu watapata fursa ya kujiandikisha kwa ajili ya usaili utakaotoa wanafunzi 60 watakaodhaminiwa kwa mafunzo hayo ya kitaalamu ya mwaka mzima yanayoendeshwa katika vituo vitatu barani afrika ikiwemo Nairobi, Lusaka na Lagos.

Kwa upande wa Tanzania, kuna nafasi nne za udhamini katika awamu hii ya pili ambapo wanafunzi hao wataungana na wenzao kutoka Kenya, Uganda na Ethiopia katika kituo cha mafunzo cha Nairobi.

Kwa wanaotaka kushiriki ni rahisi sana. tembelea  http://bit.ly/2LoDOQX  kabla ya tarehe 14/06/2019 na kisha fuata maelekezo ya namna ya kujisajili. Kwa watakaopata tatizo lolote wanaweza kutuma e-mail info@multichoicetalentfactory.com Au kupiga simu +255756753201 kwa maelekezo zaidi.

Program ya MultiChoice Talent Factory ilizinduliwa rasmi mnamo Mei 2018, kwa lengo la kuwanoa vijana wa kiafrika katika tasnia ya filamu ili kuwapa upeo, uwezo, ujuzi na weledi wa kiwango cha kimataifa katika uzalishaji na biashara ya filamu kwa ujumla.

Cituo hivyo vya mafunzo vinaongozwa na wakufunzi mahiri wenye ujuzi mkubwa na pia vina vifaa na miundombinu ya Kisasa kuwawezesha wanafunzi kujifunza uzalishaji filamu wa Kisasa na wa kibiashara.

Kama sehemu ya programu, watengenezaji wa filamu wadogo watapatiwa mafunzo na uzoefu wa vitendo katika tasnia ya filamu, kwa kuzingatia simulizi za visa, uzalishaji, sauti na kuongoza na maeneo mengine muhimu. Vituo hivi pia vinatoa fursa kwa wanafunzi ya kujifunza moja kwa moja kutoka kwa wataalamu wa sekta hiyo, kufanya kazi za kuzalisha  vipindi vya televisheni, maigizo na kuanda maudhui asilia ambayo yatakuwa yakirushwa hewani kwa njia mbalimbali ndani ya M-Net kwa kupitia  (DStv)

Darasa la kwanza la programu hii ambalo litakamilika mwezi Oktoba mwaka huu, tayari limeonyesha mafanikio makubwa ambapo wanafunzi wameshiriki katika kazi mbalimbali  ikiwemo utengenezaji wa vipindi halisia vya muziki kama Coke Studio, Pambio, Turn-Up na telenovela ya kiswahili maarufu kama Selina.

Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso, amewataka vijana wadogo kuchangamia fursa hiyo adhimu. “Nawasihi vijana wetu wa Tanzania wenye ari na nia ya kuwa nyota wa uzalishaji wa filamu duniani kuhakikisha kuwa hawakosi nafasi hii. Wajiandikishe ili waweze kupata fursa hiii muhimu”


Jiunge na mazungumzo ya mitandao ya kijamii ya MTF kwa kuandika #MultichoiceTalentFactory na jiunge:
• Instagram: @multichoicetalentfactory
• Twitter: @MCTalentFactory
• Facebook: @multichoiceafricatalentfactory


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini